Webmagic Tanzania inatafuta mfanyakazi wenye shauku ya kujaza nafasi ya Msimamizi wa Ofisi ambaye atafanya kazi za ofisini, mawasiliano na shughuli zinazohusiana na masoko.
Majukumu
- Kufanya kazi tovuti za ofisi na mteja kila siku,
- Kutengeneza na kuboresha akaunti za media za kijamii za ofisi na mteja,
- Kutangaza bidhaa na tovuti za ofisi na za wateja kwenye mitandao ya kijamii + na sehemu nyinginezo
- Kufanya mawasiliano ya kawaida kupitia barua pepe, WhatsApp, mitandao ya kijamii, SMS, simu kwa ajili ya kuwafanya wateja waendelee kuwa nasi
- Kufanya kazi nyingine za ofisi kama atakavyoamriwa na msimamizi wake
- kuwasilisha ripoti ya kila mwezi kwa msimamizi
Sifa inahitajika
- Kidato cha nne menye ujuzi na uzoefu katika tovuti na majukwaa makubwa ya mitandao ya kijamii
Sifa Zingine Zinazohitajika
- Awe na tabia ya kujitoa kufanya kazi kwa ubora
- Awe ni mtu anayewajibika na anayeaminika
- Awe ni mtu anayependa sana kutengeneza websites na mitandao ya kijamii.
- Mchapakazi anayeweza kufanya kazi nyingi, kwa ubora na kwa muda uliowekwa
- Mtu anayejali undani wa kazi na ubora kwa kazi zake zote
- Awe mtu mwenye hamu na wa haraka kujifunza na kutumia teknolojia mpya kwenye kazi zake
- Mtu mwenye fikra chanya katika maisha, juu ya wanadamu wengine na maisha kwa ujumla
- Awe ni mkazi wa jiji la Arusha
Mahali pa kazi: Arusha mjini
- Tuma ombi kabla ya tarehe 1 Agosti 2023:
- Watakao tuma mapema watafikiriwa kwanza
- Tembelea ana kwa ana au Piga/SMS/WhatsApp: 0755646470 au andika kwa info@webmagic.co.tz
- Unaweza kutembelea tovuti yetu kwa https://www.webmagic.co.tz
- Waombaji walio na sifa za msingi tu ndio watakaofikiriwa
On WebMagic Tanzania